Alexander 2nd Great

Saturday, September 14, 2013

TIMU YA SERENGETI FIESTA YATEMBELEA MASHAMBA YA WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA

Waziri Mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda (katikati), akiitembeza na kuionyesha timu ya Serengeti Fiesta baadhi ya vitu vinavyofanyika shambani hapo.

TIMU ya Serengeti Fiesta hususani iliyoupande wa kampeni ya Kamata Fursa Twenzetu, mapema leo ilipata mwaliko kutoka kwa Waziri Mkuu wa Tanzania Mh.Mizengo Peter Pinda wa kutembelea katika mashaba yake.
Timu hiyo ilifika kwenye mashamba hayo yaliyopo Kizoto nje kidogo ya mji wa Dodoma eneo la Zuzu ambalo ndilo jina halisi la mashamba hayo ambayo yanafanyika vilimo mbalimbali, ikiwemo ufugaji wa Mbuzi zaidi ya mia mbili,kilimo cha Zabibu,Nyanya,Ndizi na ufugaji wa asali.
Timu hiyo ya Clouds Group ilikuwa ikiongozwa na Mkurugenzi wa Vipindi,Uzalishaji na Mipango wa Clouds Group Rugemalila Mtahaba ‘Ruge’, ilipata fursa ya kujifunza mambo mbalimbali kutoka kwa Waziri Mkuu,hasa kuhusiana na namna ya kutumia fursa ya kujikwamua kimaisha kupitia kilimo na ufugaji.

Waziri Mkuu akimfafanulia jambo Mkurugenzi wa Vipindi,Uzalishaji na Maendeleo wa Clouds Group Ruge Mtahaba (kulia), moja ya mikakati yake ya baadae atakayoifanya shambani hapo.

Mtalamu na msimamizi Mkuu wa mashamba hayo aliyeshika chupa (kushoto), akionyesha moja ya chupa ya asali inayotengenezwa hapo.

Mtalamu wa mashamba hayo akiwatembeza na kuwapa maelezo na jinsi walivyoweza kufanikisha kilimo na ufugaji huo.
Moja ya Shamba la Zabibu likiwa katika muonekano wake.

Shamba la Nyanya likionekana.

KINANA AITEMBELEA FAMILIA ILIYOUNGULIWA NA NYUMBA SHINYANGA MJINI

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimpa pole Nassoro Rashid Tinde mmiliki wa duka la vipuri vya magari Tinde Store lililotekea kwa moto jana usiku,Shinyanga.
 Katibu Mokuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia jinsi moto ulivyoteketeza  Duka la Tinde Store  lililopo mtaa wa Nkurumah ,Shinyanga mjini kushoto ni mmiliki wa duka hilo Rashid Nassoro.
 Seif Ally akionyesha namna duka lilivyoteketea.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwapa pole majirani waliomsaidia Ndugu Nassoro Rashid kuzima moto uliounguza Duka la Vipuri vya magari pamoja na nyumba.


MTEMVU AKABIDHI MSAADA WA MAGODORO 30 HOSPITALI YA TEMEKE

 Mbunge wa temeke  Abbas Mtemvu akikabidhi kwa Lucy Sozigwa ambae ni katibu wa hospitali ya temeke  moja ya magodoro 30 yaliotolewa na kikundi cha akina mama wa  Neema Woman's Power (NWP).
 Mbunge wa Temeke Abbas Mtemvu akisalimiana na Mgeni Otto  katibu wa kikundi cha Neema Woman's Power(NWP) mara alipowasili katika hospitali ya Temeke.
 Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu akisalimiana na Moshi Ndungu ,mjumbe halmashauri tawi la Azimio.
Mbunge wa Temeke  Abbas Mtemvu akikabidhiwa magodoro 30 na Maryam Dedes ambae ni mwenyekiti wa kikundi cha Neema Woman's Power (NWP)